Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ntibanzonkiza aachwa Simba

Ntibanzonkiza Kuikosa Horoya Ntibanzonkiza kuikosa Horoya

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza, hatakuwepo katika orodha ya wachezaji 24 watakaosafiri kuelekea Guinea kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya kutokana na kuwa majeruhi.

Saido alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars uliopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Februari 3, 2023.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema Saido anaendelea vizuri na kilichomfanya asiwepo kwenye kikosi kilichosafiri ni kutokana na kutofanya mazoezi na wenzake.

Dk Edwin ameongeza kuwa Saido yupo chini ya uangalizi na ataungana na kikosi kitakaporejea nyumbani kutoka Guinea.

Wwachezaji wengine waliobaki kutokana na kutokuwa katika mpango wa mchezo ni Jonas Mkude, Peter Banda na Jimmyson Mwanuke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live