Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nsajigwa, Cannavaro walivyompigia pande staa Yanga

Shadrack Nsajigwa 2?fit=1280%2C720&ssl=1 Shadrack Nsajigwa

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna mastaa wa Simba na Yanga wanaaminiwa na uongozi hadi wanapewa jukumu la kupendekeza majina ya wachezaji wa  kusajiliwa ndani ya klabu hizo, na kama ulikuwa hujui basi kuanzia sasa elewa kwamba jambo hilo lilianza kitambo kwelikweli.

Kuthibitisha hilo, beki wa zamani wa Yanga, Godfrey Taita usajili wake kutoka Kagera Sugar 2011/12 kujiunga na klabu hiyo ulipendekezwa na Shadrack Ndajigwa na Nadir Haroub 'Cannavaro.

Akizungumzia ishu ya usajili wake Yanga, taita amesema: "Nilifuatwa na Nsajigwa na Cannavaro waliniambia mimi ni beki mzuri wanakwenda kuzungumza na viongozi, kisha watanirudia na kweli baada ya muda nikapigiwa simu ya kuhitajika Yanga."

Ameongeza: "Hao ni watu ambao nawaheshimu sana kwenye maisha yangu ya soka walifanya nipate nafasi ya kucheza Yanga, nidhamu yao iliwafanya viongozi wawaamini kwenye jukumu hilo kubwa." 

Nsajigwa kwa sasa ni kocha msaidizi wa Namungo, wakati Cannavaro maisha yake kwa sasa anaishi nchini Marekani.

Nsajigwa amekiri kuwaambia viongozi wa Yanga kumsajili Taita na walifanya hivyo, "alikuwa beki mzuri sana, ndio maana nikapendekeza jina lake."

Mwanaspoti imewahi kufanya mahojiano na Yannick Bangala kabla ya kujiunga Azam FC ambaye aliwahi kumshawishi aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi kumsajili Aziz Ki na Max Nzengeli.

"Niliwahi kumwambia kocha hao ni wachezaji wazuri na baada ya kuondoka Nabi kuna kiongozi aliwahi kuniita kujua kama Nzengeli ni mchezaji mzuri ataifaa klabu, nikamwambia wasisite kumsajili hawatajutia," amesema Bangala.

Huko nyuma iliwahi kuelezwa kwamba kabla Gadiel Michael kuondoka Simba 2023 alitakiwa kuachwa 2021/22, lakini nahodha wa timu hiyo, John Bocco aliushauri uongozi mchezaji huyo aendelee kusalia na ikawa hivyo.

Gadiel ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Cape Town Spurs ya Afrika Kusini, tangu alipokuwa amejiunga na Simba 2019 hakufanikiwa kuonyesha kiwango chake.

Pia, kipa wa Singida Fountain Gate, Beno Kakolanya aliwahi kusema: "Wakati nimesaini Singida, Bocco alitumwa na uongozi ili azungumze na mimi niweze kubakia ndani ya klabu hiyo, ila ikawa ngumu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live