Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Novautus akutana na Marseille

Novatus Dismas 40 Novautus akutana na Marseille

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ukraine kwenye timu ya Shakhtar Donetsk, atakuwa na safari yakwenda nchini Ufaransa mwakani kwa ajili ya kucheza dhidi ya Marseille kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League.

Katika droo ya michuano hii ambayo imefanyika huko Nyoni nchini Uswiss, Shakhtar ambayo imeingia kwenye michuano hii baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, inakutana na Marseille ambayo haijawahi kuchukua kombe hili licha ya kucheza fainali mara tatu, mara yamwisho ikiwa ni mwaka 2018.

Kwa upande wa Shakhtar yenyewe inaonekana kuwa na historia nzuri zaidi kwenye michuano hii kwani imewahi kuchukua ubingwa msimu wa 2008-09.

Droo yote ni hii,

Shakhtar Donetsk v Marseille

Galatasaray v Sparta Prague

Braga v Qarabag

Benfica v Toulouse

Young Boys v Sporting

Lens v Freiburg

AC Milan v Rennes

Feyenoord v Roma

Chanzo: Mwanaspoti