Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Novatus aisubiri kwa hamu Barca

Novatus Dismas 40 Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas anayeichezea FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine, amesema hesabu zao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa sasa zipo kwa miamba ya soka la Hispania FC Barcelona mara baada ya ushindi wa mabao 3-2 iliyopata juzi usiku mbele ya Royal Antwerp ya Ubelgiji.

Novatus akiwa na chama hilo jipya, alirejea Ubelgiji ambako alikuwa akiichezea Zulte Waregem kwa ajili ya kutupa karata yao ya pili kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi barani Ulaya katika ngazi ya klabu, japo0 aliishia kuwa benchi kwa dakika zote 90 za pambano hilo kali.

Licha ya mchezo huo kuwa mgumu kutokana na ubora wa FC Barcelona, Novatus anaamini wana nafasi ya kupigania matokeo ya ushindi kama ilivyokuwa dhidi ya Antwerp na kuweka hai matumaini yao ya kutinga hatua ya 16 bora.

"Kila mchezo kwenye ligi ya mabingwa ni mgumu, tulipambana sana kwa kila mchezaji kujitoa na mwishowe tukafanikiwa kupata pointi dhidi ya Antwerp ambayo ni moja ya timu kubwa Ubelgiji, naamini tutakuwa bora kama timu kutokana na maandalizi tutakayofanya," amesema nyota huyo wa zamani wa Biashara Utd.

Shakhtar Donetsk ilianza vibaya michuano hiyo kwa kukumbana na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya FC Porto wiki mbili zilizopita kabla ya kuzinduka juzi usiku dhidi ya Antwerp na sasa itarudi tena mzigoni Oktoba 25 ugenini dhidi ya Barcelona inayoongoza kundi H ikiwa na pointi sita baada ya kila timu kucheza mechi mbili.

Pamoja na kamba Novatus hakupata nafasi ya kucheza mchezo uliopita dhidi ya Antwerp, anaweza kupata nafasi dhidi ya FC Barcelona kutokana na tabia ya kocha wa timu hiyo, Patrick van Leeuwen kupenda kutoa nafasi kwa kila mchezaji kulingana na mpango wa mchezo husika.

Ikumbukwe Novatus alicheza kwa dakika zote 90 na kufanya vizuri kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa na timu hiyo na ilikuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto.

Chanzo: Mwanaspoti