Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Novatus: Sikucheza rafu, sijui refa aliwaza nini

Novats Miroshi Kadi.jpeg Novatus: Sikucheza rafu, sijui refa aliwaza nini

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Novatus Dismas Miroshi anayekipiga katika Klabu ya Shakhtar Donetsk amesema kuwa hakustahili kupewa kadfi nyekudnu katika mchezo wa AFCON jana dhidi ya Morocco.

Mwamuzi Alhadi Allaou Mahamat kutoka Chad alimlima Novatus kadi ya njano kisha nyekundu dakila ya 69 baada ya kumfanyia madhambi Azzedine Ounahi na kuufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa Stars walioambulia kichapo cha bao 3-0.

“Kila mchezaji alitamani kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu lakini matokeo yaliyokuja ni kinyume na kile tulichotarajia, kwa sasa tunajipanga na mchezo ujao dhidi ya Zambia.

“Kadi nyekundu ya leo nadhani kila mmoja aliona sidhani kama ilikuwa red card, sikumgusa mpinzani na sijui refa alikuwa anafikiria nini na kulikuwa na VAR. Kwa hiyo siwezi kusema ni uchezaji au vipi kwa sababu sikufanya faulo,” amesema Novatus.

Kiungo huyo amesema walijipanga kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Morocco na sasa watajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Zambia waweze kuondoka na pointi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live