Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Noni Madueke afikiriwa St James' Park

Noni Madueke Noni Madueke afikiriwa St James' Park

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Newcastle inafikiria kumsajili winga wa Chelsea, Noni Madueke, 22, katika dirisha hili kwa ajili ya kuongeza ubora kwenye eneo lao la ushambuliaji lililokuwa na upungufu kwa msimu uliopita.

Mabosi wa Newcastle wanataka kuipata huduma ya Noni kwa namna yoyote ambapo kama watashindwa kumnunua jumla watatuma ofa ya kwenda kumchukua kwa mkopo.

MATAJIRI wa Saudi Arabia, Al Nassr wanataka kumsajili beki wa kati wa Liverpool na Uholanzi, Virgil van Dijk mwenye umri wa miaka 32, katika dirisha hili ambapo wanataka kumpa ofa ya mshahara utakaomfanya kuwa beki anayelipwa mkwanja mrefu zaidi duniani.

Van Dijk ni mmoja kati ya wachezaji walioripotiwa kuwa wanataka kuondoka katika dirisha hili baada ya kuondoka kwa Jurgen Klopp.

MANCHESTER United inamfuatilia kwa karibu beki wa Bayern Munich na Uholanzi, Matthijs de Ligt na inataka kumsajili katika dirisha hili.

Benchi la ufundi la Man Unied linataka staa huyu asajiliwe kutokana na upungufu ambao timu yao ilikuwa nao katika msimu uliopita na taarifa zinadai beki huyu anasajiliwa kwa ajili ya kuziba pengo la Harry Maguire.

KOCHA wa Manchester United, Erik ten Hag amewaambia matajiri wa timu hiyo kwamba anahitaji huduma ya beki kisiki wa Nice na Ufaransa, Jean-Clair Todibo katika dirish hili. Todibo amekuwa akihusishwa na United tangu mwaka jana na anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kujiunga na mashetani wekundu kwa sababu mmiliki wa Nice ni Jim Ratcliffe ambaye ana hisa Man United.

AC Milan ina matumaini makubwa ya kuzipiku timu nyingine kwenye vita ya kuiwania saini ya straika wa Bologna na Uholanzi, Joshua Zirkzee, 23, ambaye anawindwa pia na Man United na Juventus. Wawakilishi wa Zirkzee wameripotiwa walikuwa England siku kadhaa zilizopita ambapo walikuwa wakifanya mazungumzo na timu mbalimbali.

JONATHAN David, ambaye anaichezea Lille pia ni mmoja kati ya washambuliaji wanaohitajika na Manchester United katika dirisha hili. Man United imepanga kufanya mazungumzo ya kina ya kumsajili fundi huyu pale itakapotuma wawakilishi wake kwenda Ufaransa kwa ajili ya dili la Jean Clair Todibo.

David alitisha kwenye Ligue 1 kwa msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 katika mechi 34.

LIVERPOOL na Manchester United zimeendelea kupigana vita kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa kati wa Lille na Ufaransa, Leny Yoro, 18, ambaye anawindwa na Real Madrid pia.

Licha ya vigogo wengi England kuonyesha nia ya kumhitaji Yoro amemwambia wakala wake kwamba anataka kujiunga na Madrid na ikiwa itashindikana ndio ataangalia timu nyingine.

Chanzo: Mwanaspoti