Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nonga, Saliboko tishio kwa Yanga

94525 Pic+nonga Nonga, Saliboko tishio kwa Yanga

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Yanga leo inaikabili Lipuli ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mabeki wa timu hiyo wanatakiwa kuwapa ulinzi Paul Nonga na Daruwesh Saliboko.

Nonga aliyewahi kucheza Yanga na Saliboko ni washambuliaji tishio katika mashindano hayo msimu huu baada ya kufunga mabao manane kila mmoja.

Meddie Kagere wa Simba anaongoza kwa kufunga mabao 12 katika mashindano hayo kabla ya mchezo wa jana ambao timu hiyo ilicheza na Polisi Tanzania.

Kocha wa Yanga Luc Eymael amekuwa akiwatumia mabeki wa kati Lamine Moro, Ally Mtoni ‘Sonso’ au Said Juma ‘Makapu’ ambaye kiasili ni mchezaji wa kiungo.

Huenda beki Kelvin Yondani aliyekosa mechi kadhaa akarejea kuikabili Lipuli kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaamm, saa moja usiku.

Nonga na Saliboko wana nafasi ya kuongeza akaunti ya mabao kwa kumpiku mshambuliaji wa Kagera Sugar Yusuf Mhilu ambaye pia ana mabao manane.

Pia Soma

Advertisement
Safu ya ushambuliaji ya Lipuli imekuwa imara kulinganisha na Yanga inayoongozwa na David Molinga mwenye mabao sita sawa na Miraji Athumani (Simba), Peter Mapunda (Mbeya City) na Reliants Lusajo (Namungo).

Katika mechi nne zilipokutana tangu mwaka 2017/2018, Yanga imeshinda mara mbili bao 1-0 na mabao 2-0, Lipuli imeshinda mara moja bao 1-0 na kutoka sare ya bao 1-1.

Msimu huu katika mechi tano za mwisho kila moja imefungwa mara mbili, imetoka sare moja na kushinda moja.

Katika mechi hizo tano, safu ya ushambuliaji ya Lipuli ilifunga mabao saba na Yanga sita. Mabeki wa Yanga wamefungwa mabao saba na wale wa Lipuli sita na washambuliaji wakipachika mabao saba.

Lipuli inayoshika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 25 ni tishio kwa kupachika mabao kipindi cha pili ambapo kati ya saba waliyofunga katika michezo mitano, matano yamefungwa kipindi cha pili dakika ya 54, 80, 75, 76, 89 na mawili kipindi cha kwanza dakika ya pili na saba.

Mabeki wa Lipuli wamekuwa wakiruhusu mabao kipindi cha kwanza, kati ya mabao sita waliyofungwa, manne wamefungwa dakika ya 7, 28, 39 na 43 na mawili dakika ya 69, 87.

Kama walivyo washambuliaji wa Lipuli, Yanga ni hatari kipindi cha pili ambapo kati ya mabao sita waliyofunga katika michezo mitano ya mwisho, matano wamefunga kipindi cha pili dakika ya 50, 51, 58, 60 na 78 na moja kipindi cha kwanza dakika ya 13.

Mabeki wa Yanga wameruhusu mabao manne kipindi cha pili dakika ya 74, 48, 74, 83, 90 na matatu kipindi cha kwanza dakika ya 25, 44 na 45.

Akizungumza jana, Nonga alisema mechi dhidi ya Yanga ni ngumu lakini watapambana kupata pointi tatu.

Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa alisema Lipuli si timu ya kubeza na leo wataingia uwanjani kucheza kama fainali.

Chanzo: mwananchi.co.tz