Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

No Pacome, no problem

Mudathir Vs Mzize Mudathir Yahya

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mudathir Yahya Abbas, simu kwa Prince Dube 'am familiar with your game', naujua huo mchezo! Pokea simu Mwana Mfalme kwakuwa Mchezaji mkubwa anapaswa kucheza timu kubwa, kushinda kikubwa na kubeba makombe makubwa! Pokea simu Prince na kama tofauti basi usisite kumpigia simu uonapo missed call ya Kiungo Mudathir.

MUDATHIR anaturejesha studio ngoma ya King Kong na Chillah! Mitaa ilisema Muda aliopoteza hawawezi kulipia, aliondoka Chamazi na kurejea kula urojo Zanzibar! Wakadhani amepotea ila Mungu wake ndie wa Mwamposa, ndio Mungu wa Isaka! From Zanzibar with Love to Jangwani kucheka na nyavu, Man on mission!

They say know your enemy! Sote tunamtambua Mudathir ni Adui wa Mabeki, kichomi kwa Makipa ila Rafiki wa nyavu! Hakuna haraka kama Bao la asubuhi la Bongo FM, hivi ndivyo vitu Extra kama Sports Xtra ya CLOUDS FM, ni Mind your Business kama Darassa! I made it kama Harmonize, Mudathir ni sanaa inayotembea yenye leseni ya BASATA, hotuba nzito baada ya kikao cha BAWACHA.

Ni siku ya Wanawake duniani, hatujatuma miamala sote tulijua zawadi zitatoka kwa Yanga Imara, zilipofika tatu tulidhani Sonara atatia nakshi kwenye mnara maarufu wa 5G! Ardhi ya Wamwera yenye Wanawake Mafundi kitandani imekutana na Yanga Afrika inayoongeza umbali wa point dhidi ya Mwekundu anayekipiga kesho Mkwakwani.

The Samson Mbangula challenge accepted! Pokea simu Afande, If you dont know about Mudathir allow us to paint the picture! Kumradhi kama English tatizo basi ulikimbia umande! Wa pili na wa tatu, njoeni vizuri Mlima huo muupande.

No Pacome! No problem! Know YANGA know Pro.

Na Farhan Kihamu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live