Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

No Haaland, No Odegaard EURO 2024

IMG 6300.jpeg Haaland na Odegaard

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara ya 12 mfululizo timu ya taifa ya Norway imeshindwa kufuzu kwenye michuano mikubwa ya Euro na Kombe la dunia baada ya kushindwa kumaliza kwenye nafasi za mbili za juu kwenye msimamo wa kundi A licha ya kubakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Scotland utakaopigwa Jumapili ya leo.

Kibaya zaidi kwa Norway wameshindwa kupata sifa ya kuwania tiketi ya Euro 2024 kupitia Playoffs, jambo ambalo linathibitisha kwenye michuano ijayo hatutawaona Erling Haaland na Martin Ødegaard ambao wanang'aa sana na vilabu vyao.

Mara ya mwisho Norway kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1998 na mara ya mwisho kuingia Euro ilikuwa mwaka 2000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live