Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nkunku asaini mkataba mpya kubaki na RB Leipzig hadi 2026

Christopher Nkunku Christopher Nkunku

Fri, 24 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Christopher Nkunku ameongeza kandarasi mpya ya kuendelea kubaki na klabu yake hiyo hadi mwaka 2026.

Nkunku ambaye ana umri wa miaka 24 amekuwa na msimu mzuri amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga msimu uliopita akifanikiwa kuisaidia klabu yake kutwaa kombe la Ujerumani maarufu kama German Cup au DFB-Pokal.

“Najisikia furaha kuendelea kuvaa uzi wa RB Leipzig. Baada ya mafanikio yetu ya kushinda kombe la DFB- Pokal ilikuwa wazi kwamba stori yangu ilikuwa bado haijatamatika katika klabu hii. Tunahitaji Zaidi ya hapa.” Alisema Nkunku.

Nkunku alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 20 na pasi 14 za mabao katika michezo 34 ya ligi kuu nchini Ujerumani na kuisaidia RB Leipzig kumaliza katika nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live