Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nkoma ataka mechi tano tu Yanga

Nkoma Pic Nkoma ataka mechi tano tu Yanga

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: eatv.tv

Siku chache baada ya kupewa mkataba wa kuiongoza timu ya wanawake ya Yanga Princess iliyopo Ligi Kuu (WPL), Sebastian Nkoma amesema amekubali kuingia makubaliano ya kuinoa timu hiyo baada ya kubaini ina kikosi kizuri na bora ambacho anaweza kukiongoza kutwaa ubingwa.

Akizungumza kocha huyo wa zamani wa Simba Queens, alisema ameingia katika timu hiyo akiwa na maswali mawili ya kujiuliza ikiwa ni pamoja na kwanini timu hiyo imeshindwa kutwaa taji ndani ya misimu minne mfululizo kwani alikuwa akiifuatilia kabla na kutamba chini yake anaamini itawezekana kwa vile ina kikosi bora.

“Ni mapema sana kuzungumza moja kwa moja nimetua kuleta taji nahitaji kukaa na timu hiyo kwa kuiongoza hata michezo mitano ili niangalie mapungufu na ubora ulipo ili niweze kuongeza nguvu yangu,” alisema Nkoma na kuongeza;

“Kuna baadhi ya wachezaji wapo nimefanya nao kazi nilipokuwa Simba kina Maimuna na sikumaliza nao vibaya ni rahisi kwangu kuanza kufanya nao kazi vizuri pia kuna wengine nimekutana nao timu ya Taifa, nahitaji kuona wanaendeleza nidhamu na ushindani ili tuweze kufikia malengo.”

Alisema nimeona usajili mzuri na naamini dhamila ya uongozi ni kubwa anahitaji kuangalia hao wachezaji ili kama wataweza kufanya kile ambacho anatamani kukiona chini yake ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la ligi ya wanawake akiwa Yanga.

Nkoma alisema atafanya kazi kwa nguvu na kuhakikisha anafikia malengo huku akisisitiza kuwaomba wanayanga kumpokea na kumpa ushirikiano ili waweze kujenga timu bora na ya ushindani.

“Natamani kuthibitisha usajili uliofanya na Yanga kwa kuchanganya wachezaji kutoka mataifa mbalimbali kama unaendana na mahitaji na kama sivyo walivyokuwa wanatarajia nitakuwa na kitu cha kuwaeleza ili tujue wapi tunaboresha zaidi na wapi tumekosea.”

Yanga Princess ilianza msimu wa WPL kwa kupigwa bao 1-0 na Fountain Gate Princess ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya Simba Queens, huku madada wa Jangwani wakimaliza nafasi ya tatu.

Chanzo: eatv.tv