Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nizar Khalfan kocha msaidizi Yanga

Khalfan EDITED 660x400 Nizar Khalfan kocha msaidizi Yanga

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Klabu ya Yanga imemtangaza rasmi mchezaji wake wa zamani na kocha wa African Lyon, Nizar Khalfan kuwa kocha wao msaidizi akiziba pengo lililoachwa na kocha Juma Mwambusi aliyejiengua hivi karibuni kutokana na sababu za kiafya.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli, Nizar amepata nafasi hiyo baada ya kupita kwenye usaili uliofanyika Ijumaa ya Januari 22, 2021.

Bumbuli amebainisha kuwa kulikuwa na makocha takribani 10 waliojitokeza kuisaka nafasi hiyo na watano walifikia hatua ya mwisho(fainali) akiwemo Salvatory Edward, Maalim Saleh na Omary Kapilima.

Chanzo: millardayo.com