Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niyonzima hana tatizo na benchi

Niyonzima Pic Data Niyonzima hana tatizo na benchi

Wed, 23 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroMore by this Author Dar es Salaam. Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Cerdic Kaze hakumaanishi kiwango kimeshuka, ila ni suala la muda.

Alisema anachokifurahi Yanga inashinda na malengo ya klabu ya kutwaa ubingwa wa msimu huu yanaendelea kuimarika.

Niyonzima, ambaye karibuni aliongeza mkataba wa miezi sita Yanga, alisema: “Ni suala la muda tu, ila sio kila mchezaji ambaye hapati nafasi ya kucheza au kuanza, hajui mpira, la hasha.

Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kuhusu yeye kuanzia benchi kwa miezi kadhaa sasa, lakini kwake anafarijika kwa timu yake inaendelea kupata matokeo.

Yanga inaongoza ikiwa na pointi 40 katika mechi 16 ilizocheza ikifuatiwa na Simba yenye pointi 32, ingawa ina mechi mbili mkononi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz