Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niyonzima ana jambo lake

Niyoo Pic Data Niyonzima ana jambo lake

Sun, 23 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema watamaliza mechi tano zilizosalia kibabe ili kujiweka katika nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.

Anaimani kubwa na timu yake kufanya vizuri katika mechi zilizosalia za lala salama ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Niyonzima alisema hadi sasa sio Simba wala Yanga ambayo inaweza ikatembea kifua mbele kwamba ana uhakika wa kuchukua ubingwa isipokuwa atakayechangisha kalata yake vyema ndiye atakokotoa pointi nyingi.

Alisema kila mmoja anamtizama mwenzake aweze kupoteza na yeye apate matokeo ili kulitwaa taji hilo la Ligi Kuu msimu huu.

“Mpaka sasa sio sisi Yanga wala Simba ambao wanauhakika wa kulitwaa taji la Ligi Kuu, ila atakayepambana zaidi atakuwa bingwa,” alisema Niyonzima. Aidha Niyonzima alisema, wao wachezaji wanajua jukumu lao nikuhakikisha wanashinda michezo yao yote ambayo imesali ili watimize malengo yao.

Niyonzima alisema, mbali na ubingwa wa ligi pia nia yao ni kulitwaa taji la FA yote yanayoshikiliwa na Simba. Yanga mpaka sasa inapointi 61 sawa na Simba ikijitupa mara 29 ikishinda mechi 17 sare10 ikipoteza mbili, huku Simba akicheza michezo 25 akishinda mechi 19 sare nne na kupoteza mbili.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz