Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niyonzima aanza na kombe Rwanda

78310 Niyonzima+pic

Thu, 3 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Yanga na Simba, Haruna Niyonzima ameanza vyema safari yake ya soka nyumbani kwao Rwanda baada ya kuchukua kombe la kwanza akiwa na klabu yake ya AS Kigali.

Niyonzima amefanikiwa kuiongoza AS Kigali kuwachapa Rayon Sport kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu zote kumaliza dakika 90 wakiwa sare ya mabao 2-2.

Niyonzima nahodha wa AS Kigali licha ya kutamba katika eneo la kiungo alifunga penalti ya pili kwa timu yake hiyo ambayo ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Amahoro unaweka historia kwa Niyonzima kuchukua taji hilo la kwanza la ngao ya jamii kuashiria ufunguzi wa ligi.

AS Kigali msimu uliopita walifanikiwa kuchukua taji la Amahoro wakati Rayon wakiwa mabingwa wa ligi kuu nchini humo.

Taji hilo linakuwa ni muendelezo wa staa huyo kuwa na bahati ya mataji ambapo kabla alitokea Simba ambako aliwapa makombe mawili ya ligi na ngao mbili za jamii katika mkataba wake wa miaka miwili.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz