Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Nishawasoma zamani, Jiandaeni kwa Ushindi" - Nabi

Nabi Pc Data Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa wanahesabu masaa tu kabla ya kuwavaa wageni kutoka Nchini Nigeria Klabu ya Rivers United katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Yanga, Nabi Nasreddine amesema kutokana na changamoto mbalimbali ambazo wamezipata wakati wa maandalizi ana imani kubwa watapa ushindi katika pambano hilo ili kurahisisha kazi katika mechi ya marudiano.

Nabi amesema kama ilivyo kawaida alitenga muda wa kutosha kuwafuatilia Rivers na kuona mambo mengi kutoka kwao jinsi ambavyo wanashambulia na kuzuia.

Amesema baada ya kuyaona hayo amerudi katika uwanja wa mazoezi licha ya kushindwa kuwa na wachezaji wote kwa ajili ya kuivaa Rivers na kuwapa mbinu za kutosha zitakazo walazimishia matokeo mazuri kwao.

“Nikuhakikishie hatukuwa na maandalizi mazuri kule Morocco pamoja na wachezaji wetu baadhi hatukuwa nao kwa pamoja kutokana na kuwepo katika majukumu ya timu zao za taifa, lakini mechi hiyo tunashinda.

“Wachezaji waliorudi kutoka katika timu za taifa wote wapo vizuri na nitawatumia, ambao watakosekana kwa sababu mbalimbali kuna mbadala wao watacheza kwenye nafasi hizo.

“Nimewajengea hali ya kujiamini wachezaji wangu pamoja na kuwapa mbinu sahihi ya kupata ushindi ili kujirahisishia kazi katika mchezo wa marudiano, kwani tunacheza na timu ngumu ambayo tunaiheshimu kutokana na ukubwa wao,” amesema Nabi.

Katika hatua nyingine, Nabi amesema wachezaji aliobaki nao ambao hawakuwa katika majukumu ya timu za Taifa wengi wamefanya mazoezi kwa ubora wa hali ya juu katika kutimiza majukumu yao, jambo linalomtibitishia kuwa hawatakua na huruma siku ya Jumapili.

Nabi amesema kwa kujiamini kuwa kwa muda aliotumia kuwasoma wapinzani wao, na namna alivyowapa majukumu ya kukabiliana nao wachezaji wake haoni ni namna gani watashindwa kuibuka na ushindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live