Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ninja kumwaga wino leo Lubumbashi

Ninja Shaibu Aliyekuwa beki wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja'

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa beki wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' ametua DR Congo kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Lubumbashi Sport ambayo imempa ofa ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka DR Congo beki huyo atasaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na timu hiyo ya Lubumbashi leo, Ijumaa baada ya jana, Alhamisi kuonyeshwa mazingira ya chama hilo.

Akiongelea dili hilo, Ninja alithibitisha kusafiri lakini alificha sehemu aliyopo huku akiomba muda wa kukamilisha kilichompeleka huko, ikimbukwe kuwa awali beki huyo alikuwa kwenye rada za Geita Gold.

"Sipo Tanzania nimesafiri kidogo, nipo kwenye mchakato wa kukamilisha usajili wangu, kila kitu kikiwa sawa nitawaweka wazi timu ambayo nitaichezea kwa ajili ya msimu ujao," alisema beki huyo.

FC Lubumbashi Sport ambayo Mwanaspoti inafahamu kuwa Ninja ataichezea, imevutiwa na kiwango chake na inaamini kuwa nyota huyo atakuwa msaada kutokana na uzoefu alionao.

Chanzo chetu kinaeleza,"Kulikuwa na vikao viwili, ndani ya timu yupo mtu ambaye anaijia vizuri ligi ya Tanzania ndio maana imekuwa rahisi kupitishwa wanajua uwezo wa mchezaji na uzoefu aliona."

Msimu uliopita kabla ya ligi kuu nchini humo kuvunjika kutokana na kukosekana kwa mdhamini, FC Lubumbashi Sport ilikuwa ikishika nafasi ya 14 kati ya timu 20 walicheza michezo 10 na kuvuna pointi tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live