By Mwanahiba RichardMore by this Author Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu amesema kuwa isingekuwa rahisi kwa straika wa Simba, Meddie Kagere kufurukuta mbele yake hasa akiwa anacheza kwenye ardhi yake ya nyumbani.
Ninja alikuwa sambamba kila hatua ambayo Kagere anapiga katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi ililofanyika juzi Jumatano kwenye uwanja wa Amaan kisiwani hap ambapo Yanga walitwaa ubingwa huo.
Yanga walitwaa ubingwa huo kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya dakika 90 kutoka sare tasa hivyo bingwa kupatikana kwa penati.
Ninja ambaye alipiga penati ya pili kati ya tano zilizokuwa zimepigwa kwa kila timu lakini beki huyo na mwenzake Said Juma Makapu wakimbada vilivyo Kagere aliyeonekana kushindwa kupenya mbele yao.
Ninja alisema kuwa Kagere ni mchezaji mzuri hivyo unapaswa kuwa makini kucheza naye na kutompa nafasi ya kupita anapokuwa kwenye eneo la hatari.