Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nini kimempata Kipre Jr?

Kipree  WA0003 Nini kimempata Kipre Jr?

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Azam FC, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon 'Kipre JR' mechi tano za mwisho kabla ya Ligi kusimama alikuwa moto haswa akifunga mabao na kutengeneza mabao .

Kipre aoja ya wachezaji ambao wanatajwa zaidi pale Azam Football Club huku kasi yake na ufundi wake ulisababisha timu yake iwe na matokeo bora katika michezo ya NBCPL.

Sasa ni mchezo wa tatu mfululizo Kipre JR tangu Ligi imerejea tena ule ubora wake wa kutunza Mpira haupo tena umakini nao umeondoka, miguu yake haina macho tena.

Inaonyesha Kipre JR kipindi cha mapumziko ya AFCON alijisahau sana hali iliyo sababisha asitunze ule ubora wake ambao alikuwa nao hapo awali.

Azam walikuwa wanategemea ubora wa Kipre JR na Sillah Ili kutengeneza mabao kwa sasa wote Kasi yao imepungua Hali inayo sababisha safu yao ya ushambuliaji ishindwe kutengeneza nafasi za kutosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live