Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nini cha kutarajia kutoka kwa Real Madrid 2022/23

Madrid22411 Nini cha kutarajia kutoka kwa Real Madrid 2022/23

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Hispania na Ulaya, huwa wanatarajiwa kushinda kila mashindano wanayoshiriki.

Msimu huu si tofauti kwani Kocha Carlo Ancelotti atakuwa akitafuta kunyakua angalau mataji mawili makubwa baada ya kubeba taji la Klabu Bingwa Dunia juzi kwa kuifunga Al Hilal ya Saudi Arabia kwa mabao 5-3 katika mchezo wa fainali uliopigwa Morocco.

Ligi ya Mabingwa Ulaya ni shindano ambalo 'Los Blancos' wana rekodi ya kushangaza na mabingwa hao watetezi wanatarajia kurudia ushujaa wao wa msimu uliopita. Ancelotti pia atajaribu kumaliza ukame wa klabu hiyo wa Copa Del Rey.

Mashabiki wa Madrid wangependa kuona timu yao ikinyanyua Kombe la Copa del Rey mwaka huu.

Mwaka huu unaweza kuwa hadithi tofauti kwani tayari wako kwenye fainali ya shindano hilo dhidi ya Barcelona Machi 2, mwaka huu.

Los Blancos hao walifedheheshwa na Barcelona walipopoteza kwa mabao 3-0 kwenye Supercopa de Espana mapema mwezi huu.

LIGI YA MABINGWA ULAYA

Real Madrid walikuwa na moja ya mbio bora zaidi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita huku wakizishinda timu zote bora kwenye dimba hilo na kushinda taji hilo kwa mara ya 14.

Uchezaji wao msimu huu umekuwa wa kuridhisha pia, kwani waliongoza kundi lao. Madrid itacheza na Liverpool katika Raundi ya 16-Bora katika mechi ya marudiano ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2022, ambayo Los Blancos ilishinda 1-0. Mechi ya kwanza itachezwa Februari 21 kwenye Uwanja wa Anfield.

LALIGA

Ligi Kuu Hispania, LaLiga imeonekana kushuka kwa ubora katika miaka michache iliyopita tangu Cristiano Ronaldo na Lionel Messi waondoke. Barcelona na Real Madrid ziko katika kinyang'anyiro cha kuwania taji la ligi msimu huu.

Real Madrid ilishinda LaLiga kwa raha msimu uliopita ikiwa na faida ya pointi 13 dhidi ya Barcelona. Mwaka huu, wanaburuza mkia kwa Barca kwa pointi nane kabla ya mechi za jana.

Ingawa Madrid waliwashinda Barcelona kwa raha katika mechi yao ya LaLiga, wamepoteza pointi mara nyingi sana. Barca hawaonyeshi dalili za kupunguza kasi, hivyo Real Madrid wanatakiwa kuwa katika ubora wao ili kuendelea kuwa karibu na wapinzani wao hao.

WACHEZAJI WANAOWAHITAJI

Vinicius Junior na mshindi wa Ballon d'Or, Karim Benzema ndio silaha kubwa zaidi kwa Real Madrid. Watalazimika kuendelea kucheza kwa kiwango sawa na msimu uliopita ikiwa wanataka timu yao kufikia mafanikio.

Vinicius alionyesha dalili za wasiwasi katika sehemu za mwanzo za msimu, lakini winga huyo amerejea kufanya kile anachofanya vema zaidi. Benzema amekuwa butu tangu kuumia kabla ya Kombe la Dunia. Amefunga mabao tisa kwenye LaLiga, manne chini ya mabao 13 ya Lewandowski. Itakuwa vigumu kwake kushinda tuzo ya mfungaji bora (Pichichi) kwa kasi hii.

Hata hivyo, anazidi kushika kasi na bao lake dhidi ya Atletico Madrid katika robo fainali ya Copa del Rey hakika litampa nguvu ya kujiamini. Thibaut Courtois yuko katika kiwango kizuri, kama vile msimu uliopita, ambao ulikuwa bora kwake binafsi.

KIWANGO

Los Blancos wameshuka ghafla katika hali yao tangu mapumziko ya Kombe la Dunia. Walichapwa na Villarreal na FC Barcelona katika muda wa siku tisa. Real Madrid walipata ushindi usioridhisha dhidi ya Real Valladolid, CP CacereƱo na Valencia.

Walishinda 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao wakiwa ugenini, ambayo ni mafanikio makubwa ukizingatia kiwango chao cha hivi majuzi na walitoka suluhu na kufanya matokeo kuwa 3-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Kuna baadhi ya masuala ambayo Ancelotti anahitaji kutatua haraka iwezekanavyo. Vinicius anatengwa mara nyingi sana kwenye ubavu wa kushoto na Ferland Mendy anapaswa kufanya zaidi kumsaidia katika kushambulia. Pia Rodrygo anastahili kupata muda zaidi wa mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live