Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nini Pacome? Chama anazidiwa hata na Mudathir - Shabiki Simba

Chama Mudathir Pacome Nini Pacome? Chama anazidiwa hata na Mudathir - Shabiki Simba

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa ni kosa kubwa kumfananisha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua na kiungo wa Simba, Clatous Chama kwani Mzambia huyo kwa sasa ni kama amekwisha.

Mchome amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa, Chama anazidiwa hata na Mudathir yahya Abbas hivyo, nyota huyo wa Simba anapaswa kujitafakari na kurejesha kiwango chake badala ya kuingia kwenye migogoro na timu yake.

“Sio sahihi kumfananisha Chama na Pacome kwa sababu Pacome kwanza ndiyo msimu wake wa kwanza na umekuwa na mafanikio makubwa mno. Chama anayezungumzwa siyo chama huyu, ni Chama wa misimu mitano mine nyuma.

“Chama huyu ni uji uji, Chama huyu huwezi kumfananisha hata na Mudathir Yahya Abbas kwa sababu Mudathir ana goli la CAF, lakini Chama hana.

“Kwenye Ligi Kuu, Mudathir ana mabao sita, anamzidi Chama ana mabao matatu. Kwa hiyo mtu wa kumfananishwa na Chama siyo Pacome, ni mUdathir Yahya. Pacome amemwacha Chama mbali sana. Namba za Mudathir zimemwangusha Chama.

“Mudathir tu hamkamati, sasa utamlinganishaje na Pacome. Niseme tu kwamba, Chama ajitathmini, aache mgongano na viongozi, afanye kazi iliyompeleka Simba, tofauti na hapo heshima yake inaanguka,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live