Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nini Benchikha? Hata akija Guardiola Simba hatutoboi - Shabiki

Benchikha Simba Ms Nini Benchikha? Hata akija Guardiola Simba hatutoboi - Shabiki

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa ubora wa kocha mpya wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha utaangushwa na aina ya wachezaji waliopo katika kikosi hicho kwani hawajitumi.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kuwa na matokeo mabovu ambapo katika mechi tatu za mwisho kuanzia kipigo cha bao 5-1 kutoka kwa watani zao Yanga, sare ya bao 1-1 na Namungo na sare ya bao 1-1 na ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

"Kocha Benchikha ana profile nzuri sana na mara nyingi Simba kinachotugharimu ni profile. Yani namba za watu huwa zinatudanganya sana kwenye suala la usajili. Tumemsajili Onana, alikuwa MVP huko alikotoka, tumemsajili Che Malone alikuwa MVP kule alikotoka lakini wako wapi? Wanapoteana.

"Kwa hiyo hili sauala la kuwa na kocha mzuri linategemeana na kikosi alicho nacho, USM Alger ilikuwa na vijana wadogo wanaojituma huwezi kulinganisha na hii Simba. Kama amekuja nadhani atachukua nafasi ya kusajili wachezaji anaowataka lakini wakimwachia wachezaji hawa hawa waliopo kwa sasa waliochoka, tutaadhibiwa na kocha wetu huyu.

"Labda arudishe morali lakini kwa wachezaji waliopo hata wamlete kocha wa Man City, Pep Guardiola bado watamwangusha kwa sababu wachezi hawajitumi. Wakitoka uwanjani hamna hata jasho utadhani wametokagesti au baa.

"Viongozi waandae mazingira ya kujua kuwa mchezaji ni mwajiriwa wa klabu anaweza kutoka muda wowote akaja mwingine," amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live