Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimeshawasoma Yanga, nitacheza na madhaifu yao - Kocha Mamelodi

Bacca X Job X Mokwena Nimeshawasoma Yanga, nitacheza na madhaifu yao - Kocha Mamelodi

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Mamelodi Sundwons, Rhulani Mokwena amesema mechi yao ya leo dhidi ya Yanga SC itakuwa ni ya kuvutia kwani wanaenda kucheza dhidi ya timu bora ambayo inafanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Mokwena amesema mwaka jana Yanga wamefika kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na msimu huu wamefuzu hatua ya mtoano kutoka kwenye kundi gumu lenye timu zoefu.

Mokwena ameongeza kuwa Yanga inafundishwa na kocha mzuri Miguel Gamondi na ina wachezaji wazuri kutoka Tanzania na wengine kutoka mataifa mengine ya Afrika kama Aziz Ki anayetokea Burkina Faso.

“Tunatarajia mechi ngumu kesho (leo), lakini sisi tupo tayari”.

Mokwena alipoulizwa kuhusu ataweza vipi kuipita safu ya ulinzi ya Yanga SC ambayo inakabia chini bila timu yake kuacha nafasi nyuma ambazo Yanga wanaweza kuzitumia kwenye “Counter Attack”

Mokwena amejibu kuwa hapo ndipo mechi ilipo kesho na kusema watapaswa kutafuta mashimo kwenye safu ya ulinzi ya Yanga ili kuivuka, na tayari wameshafanya uchambuzi na wachezaji wake wameelewa ugumu wa mechi hiyo upo wapi.

"Nmerudia kuangalia mechi zao, Yanga wana mabeki wazuri, Dickson Job, Ibrahim Bacca, viungo wazuri Khalid Aucho ambaye mchezo huu tunaamini ataanza baada ya kuukosa mchezo uliopita, Mudathir Yahya kama namba 8.

"Aziz Ki kama namba 10 na Kennedy Musonda ambaye anapenda kupitia pembeni kulia au kushoto pale ambapo mabeki wetu wanaacha nafasi akisaidiana na Clement Mzize, mechi itakuwa ngumu ila tumeshawasoma Yanga na tunajua cha kufanya, wachezaji nimeshawaelekeza kilichobaki ni kutekeleza mpango wetu," amesema Mokwena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live