Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimependa usajili wa Yanga - Shaffih Dauda

Chama Yanga 003 Clatous Chota Chama.

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya Soka kupitia Clouds FM kipindi Hili Game, Shaffih Dauda amesema kuwa amependa aina ya usajili wa wanaoufanya Yanga na kuwabakisha nyota wake wake muhimu.

Dauda amesema hayo baada ya Yanga kumsajili aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama huku kukiwa na tetesi za kumsajili mshambuliaji Prince Dube ambaye ameshavunja mkataba wake na Azam FC.

“Nimependa namna Yanga wanavyosajili, wachezaji wao muhimu wote wamefanikiwa kuwabakisha, bila shaka hawa wachezaji wameonesha uwezo mkubwa sana mtu kama Aucho haimbwi vile inavyotakiwa lakini ameonesha kiwango cha juu sana.

“Tumezoea kuwaimba wachezaji wanaofunga tu , tuzo za mwezi wanapewa wafungaji Aucho anaathirika kwa mentality hiyo ambayo atazungumzwa zaidi Aziz Ki , Feisal ambao wanafunga magoli,” amesema Shaffih Dauda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live