Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimekuwa mwalimu kwa miaka 12, nikatumbuliwa na Magufuli - GB64

Gb64 Teacherz Nimekuwa mwalimu kwa miaka 12, nikatumbuliwa na Magufuli - GB64

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba SC, Abdul Shaibu Hega maarufu kama GB6 amefunguka kuwa mbali ya ushabiki wa soka yeye kitaaluma ni Mwalimu wa masomo ya Fizikia, Jiografia na Hesabu, kazi ambayo ameitumikia kwa miaka 12.

Shaibu ameongeza kuwa, ujio wa madarakani wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika harakati za kutumbua watumishi hewa wasio na vigezo, GB64 naye alipitiwa na fagio hilo huku akidai kuwa anatamani kujiendeleza lakini hana uwezo wa kifedha

“Majina yangu kamili ya NIDA ni Abdul Shaibu Hega maarufu kama GB64 Genuine. Nimeanza kushabikia mpira tangu nikiwa na umri wa miaka 6. Baba yangu alikuwa shabiki lialia wa Simba na alicheza Tanzania Breweris kama beki wa kati.

“Jina la GB64 alinipa Ahmed Ally (Meneja habari na Mawasiliano wa Simba SC), kabla ya hapo nilikuwa naitwa Teacher ukija pale Karume watakwambia kwa sababu mimi kwa taaluma ni mwalimu wa Physics na Hesabu. Crash program ya kwanza sisi ndiyo wazidnuzi wa shule za kata lakini alipokuja rais Magufuli akasema vyeti vyetu vya crash program havitambui, tukatumbuliwa na kazi ya ualimu ikaishia hapo.

“Nimefundisha miaka 12 tangu mwaka 2006. Magufuli alipotutumbua akasema turudi chuoni tukasome, sasa unakuta una familia uki-apply Bodi ya Mikopo wanasema ujisomeshe mwenyewe, ikabidi turudi mtaani tuanze kufanya shughuli nyingine. Mimi ukiniletea mtoto namfundisha kuanzia form 1 hadi form 4 bila kitabu.

“Mimi ni mwalimu bora na mwalimu wa mfano na ninapenda kazi ya ualimu, Nilichukua Physics, Geography na Hesabu (PGM), hayo masomo matatu niko vizuri sana,” amesema GB64.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live