Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Nimejiunga na klabu kubwa Afrika" - Banda

Peter Banda 2?fit=1080%2C719&ssl=1 Kiungo mshambuliaji wa Simba, Peter Banda

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Winga mpya wa Simba, Peter Banda amezungumzia mipango yake ndani ya klabu hiyo akieleza Simba ni miongoni mwa timu nne kubwa barani Afrika sawa na Al Ahly ya Misri na Mamelody Sundowns ya Afrika Kusini.

Banda aliyesajiliwa na Simba katika dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea Sheriff Tiraspol ya Moldova alikokuwa kwa mkopo akitokea Nyassa Big Bullets ya Malawi ameeleza kuwa ukubwa wa Simba ni miongoni mwa sababu zilizomfanya ajiunge na Wekundu wa Msimbazi.

“Nafurahi kuwa hapa. Nilitamani kucheza katika timu kubwa kama Simba kwani nilianza kuisikia tangu nina miaka 15 nikiwa nyumbani Malawi,” amesema.

“Nilichagua kujiunga Simba na kuachana na timu nyingine za Ulaya zilizonitaka kwa sababu timu hii ni kubwa zaidi na kwa sasa ni miongoni mwa timu tatu au nne kubwa Afrika sawa na Ahly na Mamelody.”

Pamoja na hayo, Banda alieleza malengo yake ndani ya Simba na kufunguka kuwa amekuja kuipa makombe na kuifanya ifanye vizuri katika michuano yote inayoshiriki.

“Nimepanga kuwaonyesha mashabiki kuwa nina uwezo mkubwa, pia kuwathibitishia mashabiki waliobeza usajili wangu. Nataka niisaidie Simba kushinda Ligi Kuu Bara na kuifanya ifike juu zaidi kwenye michuano ya kimataifa, kwani naamini uwezo huo tunao,” amesema Banda.

Ameweka wazi kuwa alifurahia mapokezi yake na sasa ameanza kujifunza Kiswahili na maneno yake ya kwanza kuyajua ni “mambo, poa na mwanangu” kwa sababu akiwa mazoezini ndio anayasikia mara kwa mara.

Chanzo: Mwanaspoti