Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nilichokiona Coastal Union vs Yanga

Moloko, Mzize Walivyoinusuru Yanga CCM Mkwakwani.jpeg Nilichokiona Coastal Union vs Yanga

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sio mara yakwanza, ni kama mazoea ndani ya Ligi yetu kila baada ya mchezo wa dabi ya Kariakoo lazima mapacha wa Kariakoo wapitie mfupa mguu wa kutafuna na hiyo inasababishwa na matumizi makubwa ya nguvu kwenye mchezo huo .

Game plan ya kwanza ya Coastal Union dhidi ya Yanga jana hii ilikuwa ni kuinyima Yanga urafiki na mpira, walikuwa wanafika sana kila eneo ambalo Yanga ilikuwa inapeleka mpira na wanafanya pressing kiumakini.

Mbinu ilitiki sana kwa asilimia kadhaa maana wachezaji wengi wa Yanga hawakuwa vizuri kwenye upokeji wa mpira sababu ya uchovu hususani kipindi cha kwanza Coastal walitumia nguvu kubwa sana kwenye kuinyima uhuru Yanga, well done Coastal Union.

Coastal Union game plan yao iliharibika kipindi cha pili, pale tu ambapo walitaka kuilinda sare dhidi ya mpinzani mgumu.

Yanga walianza kuwa rafiki na mpira ilianza kusogea kwenye lango la Coastal kwa uhuru sana na Miguel Gamondi alifanya mabadilko ya Mzize na Moloko ambao hawakutumika sana kwenye dabi na bado walikuwa na njaa. Well done Gamondi wote wamehusika kwenye bao la Yanga, ubora ndani ya kikosi.

Kipindi cha kwanza kiliisha lakini timu zote mbili ulikuwepo ulazima wa kadi nyekundu, tukio la Ibrahim Ajibu na Khalid Aucho. Ilibidi Ajibu apewe kadi ya njano na Aucho apewe kadi nyekundu, lakini makosa ya kibinadamu ya Mwamuzi yalibalansi mambo.

Pia, kuna tukio la Kennedy Musonda kupigwa ngumi na mchezaji wa Coastal ile pia ilikuwa ni Red Card kwa Mchezaji wa Coastal Union.

Clement Mzize, Super sub anatokea nje dhidi ya Simba anakiwasha sana, ameingia jana amefunga moja ya hadhina kubwa ya Taifa kuelekea AFCON.

Lucas Kikosi 'Almeda' hadithi yako tungeumia kama ingeishia Namungo, yule Kikoti huenda anaweza kurudi. Matokeo ni ya timu nzima lakini performance binafsi ni alama kwa Mchezaji.

Full Time

Coastal 0 ➖ Yanga 1

Clement Mzize ⚽

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: