Nike imetoa ufafanuzi kuhusu Mason Greenwood baada ya nyota huyo kuonyesha viatu vyake vyenye nambo ya kampuni hiyo kipitia akaunti yake ya Instagram.
Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 22 aweka picha yake ikimuonyesha amevaa kiatu cha Nike na kuzua maswali kwa mashabiki.
Greenwood alizua gumzo kutokana na picha hiyo ikimuonyesha akiwa na lundo la viatu tofauti kwenye bei yenye nembo ya Nike, pia picha moja ilionyesha jozi ya viatu yenye thamani ya Pauni 9,000 aina ya “Platinum Nike Dunk Lows”.
Kabla ya Greenwood kukamatwa kutokana na shutma ya za kumpiga mpenzi wake na kutishia kuua, nyota huyo alikuwa anadhaminiwa na kampuni Nike.
Lakini baada ya sakata hilo kutokea Nike ilisitisha mkataba wake wakati kesi yake ikiendelea, hata hivyo, mashtaka yote ambayo Greenwood amekuwa akihusishwa nayo yalifutwa Februari 2023.
Sasa, kampuni hiyo kubwa ya mavazi ya michezo imethibitisha kuwa Greenwood sio balozi wa Nike, licha ya chapisho la hivi karibuni: “Mason Greenwood sio sehemu ya familia ya Nike tena,” msemaji wa kampuni aliiambia The Sun.
Wakati huo huo, Greenwood bado hajapata shavu la kudhaminiwa tangu Nike ilipovunja mkataba naye. Hii ina maana kwamba mshambuliaji yuko huru kusaini na kampuni yoyote yenye upinzani na Nike
Imefahamika wachezaji ambao hawana mikataba ya ufadhili na kampuni mara nyingi wanapenda kuvaa viatu vyeusi ambavyo havina nembo.
Mfano nyota wa Real Madrid, Vinicius Jr aliwahi kuvaa viatu vyeusi alipokuwa na mgogoro na kampuni ya Nike msimu uliopita.
Greenwood tangu alipotua Getafe kwa mkopo akitokea Manchester United, amefunga mabao matatu na asisti tatu