Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria, Tunisia zapewa vigogo 16 bora Kombe la Dunia U-20

Nigeria U20 Nigeria, Tunisia zapewa vigogo 16 bora Kombe la Dunia U-20

Mon, 29 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nigeria na Tunisia zimefuzu hatua ya 16 Bora ya Fainali za Kombe la Dunia za Vijana umri chini ya miaka 20 baada kupitia kwenye kapu la washindwa bora, lakini zote zimejikuta mikononi mwa vigogo.

Fainali hizo za 24 zinapigwa nchini Argentina na bara la Afrika likiwakilishwa na nchi nne zikiwamo Gambia na Senegal ambayo imeishia hatua ya makundi kwa kuburuza mkia katika Kundi C.

Senegal ndio mabingwa wa Afrika U20 2023 baada ya kuifunga Gambia kwenye fainali, huku Nigeria ilimaliza ya tatu ikiifunga Tunisia katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Nigeria iliyokuwa Kundi D katika fainali hizo za Argentina ikiwa pamoja na Brazili na Italia, imepangwa kuvaana na mabingwa wa kihistoria, Argentina, huku Tunisia iliyomaliza ya tatu katika Kundi E lililokuwa na nchi za England na Uruguay yenyewe imepewa Brazili.

Mwakilishi mwingine wa Afrika, Gambia iliyomaliza kama kinara wa Kundi F ikizitangulia Korea Kusini na Ufaransa sasa itakutana na Uruguay katika hatua hiyo iliyopangwa kuanzia kesho Mei 30, ili kusaka timu nane za kutinga robo fainali.

Mechi nyingine za 16 Bora itazikutanisha nchi za USA na New Zealand, Colombia dhidi ya Slovakia, England itaumana na Italia, Ecuador itavaana na wanafainali wa 2019, Korea Kusini na mechi nyingine itakuwa ni kati ya Uzbekistan na Israel.

Fainali zilizopita za michuano hiyo, zilizofanyika Poland 2019, Ukraine ndio iliyobeba taji ikiifunga Korea Kusini kwa 3-1. Hata hivyo, Ukraine safari hii haikufuzu fainali hizo za Argentina.

Chanzo: Mwanaspoti