Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nidhamu ndio silaha ya Yanga kuipiga TP Mazembe

Yanga Squad Tunis.jpeg Sehemu ya kikosi cha wachezaji wa Yanga

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyotawa kimataifa wa zamani aliyewahi kukipiga Yanga, Mtibwa Sugar na Taifa Stars, Abdi Kassim 'Babi', ameweka wazi kwamba mastaa wa Yanga watacheza kwa nidhamu ya hali ya juu mbele ya TP Mazembe basi kuna uwezekano mkubwa wa kubeba pointi tatu nyumbani.

Yanga inaikaribisha Mazembe kwenye mechi ya Kundi D ya Kombe la Shirikisho Afrika itkayochezwa kuanzia saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na Babi aliyewahi kucheza soka la kulipwa nchini Malaysia, alisema anaipa nafasi kubwa Yanga kushinda.

Kiungo mshambuliaji hiyo anayeshikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ulipozinduliwa kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Taifa Stars na Uganda The Cranes mwaka 2007, alisema nidhamu ndio itakayoibeba Yanga.

Babi aliliambia Mwanaspoti, mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote lakini anachoamini kama Yanga wataingia kwa nidhamu na kuwaheshimu wapinzani wao wenye uzoefu mkubwa na mashindano hayo basi wanaweza kuibuka na ushindi.

“Kikubwa wachezaji wa Yanga watambue kwamba wapo kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki sasa utawafurahisha vipi ndio hiyo lazima upambane ili uweze kuibuka na ushindi ambayo ndio muhimu kwa sasa kwao,” alisema Babi.

Aliongeza mechi kama hizi zenye presha kuanzia nje na ndani ya uwanja zinahitaji mchezaji kuwa makini kwa hali ya juu kwani unaenda kucheza na timu ambayo ina ubora kuliko timu yako lakini pia ukiangalia wewe umetoka kupoteza mchezo uliopita.

Alisema kama mashabiki pia watajitokeza kwa wingi na kuujaza uwanja unaweza kuwa ni faida nyingine kwa upande wa Yanga kwa maana kuanikiza na kuongeza nguvu uwanjani ili wachezaji wapate nguvu na morali ya kupambana katika mchezo huo.

Chanzo: Mwanaspoti