Mshambuliaji wa Chelsea, Nicolas Jackson, amesema amefurahi kufunga mabao matatu ‘hat-trick’, katika mchezo wa Ligi Kuu England hidi ya Tottenham, juzi Jumatatu (Novemba 06).
Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja Tottenham, Jackson alifunga mabao hayo katika ushindi wa 4-1.
Mshambuliaji huy9o kutoka nchini Senegal amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga ‘hat-trick’ dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu England tangu Jimmy Hasselbaink alipofanya hivyo mwaka 2002.
Jackson amesema amefurahi kuisaidia timu yake kupata ushindi huo, lakini pia anapaswa kuboresha kiwango chake ili kuwa na makali zaidi.
“Nina furaha sana, awali ulikuwa wakati mgumu kwa kila mtu katika timu. Tunarudi katika ubora wetu kidogo kidogo na nina furaha kufunga mabao matatu.
“Ni hat-trick yangu ya kwanza, hivyo nina furaha kufanya hivyo nikiwa na timu kubwa England na kila mahali,” aliambia Sky Sports.
Nyota huyo aliongeza kuwa: “Nahitaji kuendelea kuboresha kujituma zaidi. Tunaendelea kufanya kazi,”
Mchezaji huyo amejiunga na Chelsea msimu huu akitokea Villareal ya Hispania kwa Pauni Milioni 32.
Hadi sasa, mchezaji huyo amefunga mabao matano katika mechi 10 za Ligi Kuu ya England.