Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nico Williams awekwa kwenye rada Arsenal

Nico Williams Athletic Club 2023 24 1714729607 135650 Nico Williams

Sat, 24 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga Mhispaniola, Nico Williams ameripotiwa kuingia kwenye rada za miamba ya soka ya Emirates, Arsenal na huenda ikanasa saini yake kwenye dirisha hili kabla halijafungwa, Agosti 30.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 22 alionyesha kiwango bora sana kwenye kikosi cha La Roja katika fainali za Euro 2024 zilizofanyika Ujerumani na kuisaidia timu yake ya Hispania kunyakua ubingwa.

Alifunga mabao mawili katika fainali hizo, moja likiwa kwenye mchezo wa fainali dhidi ya England.

Kiwango chake bora kilivutia timu kubwa za Ulaya, ikiwamo Barcelona, Chelsea na Liverpool miamba miongoni mwa vigogo waliokuwa wakifukuzia huduma ya mkali huyo wa Athletic Bilbao.

Lakini, kwa mujibu wa The Independent, Arsenal anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuwa wao wa kwanza kunasa saini yake.

Williams inafahamika wazi amekuwa kwenye rada za Arsenal katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa dirisha la usajili.

Winga huyo mwenye mkataba wake inaelezwa kuna kipengele kinachohitaji ilipwe Pauni 48 milioni tu kumsajili, kitu ambacho kinadaiwa ni bei ya chini sana kutokana na hali ilivyo kwa sasa kwenye soko la usajili.

Hata hivyo, kwa kipindi hiki mwenyewe bado amekuwa akisita kuachana na Athletic Bilbao. Williams alikabidhiwa jezi Namba 10 na klabu yake wiki iliyopita huku akiwahi kuweka wazi ndoto zake za kwenda kujiunga na Barcelona. Na sasa kama Arsenal itashindwa kumnasa Mhispaniola huyo kabla ya dirisha kufungwa Ijumaa ijayo, watakuwa wamebadili mipango yao, ambapo kwa sasa wanataka mtu wa kuja kuleta ushindani wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza na si wa kuanzia benchini kama Leandro Trossard.

Mbelgiji Trossard alijiunga na Arsenal kwa ada ya Pauni 27 milioni akitokea Brighton kwenye dirisha la Januari mwaka jana, wakati miamba hiyo inayonolewa na Mikel Arteta kushindwa kumsajili Mykhailo Mudryk. Trossard tangu wakati huo amefunga mabao 18 na asisti 12 katika mechi 69.

Mchezaji mwingine ambaye Arsenal wanaamini anaweza kufiti kwenye mipango yao ni Ademola Lookman. Kwenye dirisha hili, Arsenal imesajili beki Riccardo Calafiori kutoka Bologna kwa ada ya Pauni 42 milioni na iliripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili la kiungo Mikel Merino kutoka Real Sociedad, ambaye ameripotiwa atawagharimu Pauni 33 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti