Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni wakati sasa wa waamuzi wetu kujiongeza

Waamuzi Zz.jpeg Ni wakati sasa wa waamuzi wetu kujiongeza

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ukiangalia orodha ya waamuzi wengi wanaopangwa kuchezesha mechi za kimataifa zilizo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) na lile la Afrika (Caf) utagundua mambo mawili kwa wengi.

Kwanza wengi ni watu ambao wana ajira rasmi na zenye hadhi fulani katika jamii hasa zile za umma na kwa taasisi kubwakubwa. Kuna haja ya marefa wetu nao kujiongeza kitaaluma ili kudaka fursa nyingi zaidi.

Kuna walimu, madaktari, askari, wanasheria, wahasibu, wasanifu, wataalam wa kompyuta, waandishi wa habari, wahandisi na kadhalika.

Mfano, refa wa Ethiopia, Bamlak Tessema kitaaluma ni mtafiti akiwa na shahada ya uzamili aliyopata katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa wakati refa Mohamed Adel wa Misri ni askari polisi.

Lakini ukiondoa suala la kazi, kuna hili la taaluma hasa uwezo wa kuzungumza lugha nyingi za kimataifa ambalo nalo limezingatiwa.

Marefa wenye uwezo wa kuzungumza vizuri lugha za Kiingereza na Kifaransa hata Kiarabu wamekuwa wakipewa kipaumbele zaidi kulinganisha na wale wa lugha nyingine.

Yule Pacifique Ndabihawenimana wa Burundi anaongea vizuri tu Kifaransa, Kiingereza, Kiarabu na anamudu pia kuzungumza lugha ya Kiswahili.

Katika hali ya kawaida huyu atakuwa na nafasi kubwa ya kuteuliwa kuchezesha mechi za kimataifa kuliko mwenzangu na mimi ambaye anatamba na Kiswahili tu.

Kuna haja pia kama nchi kuangalia jinsi ya kuboresha zile njia ambazo tunatumia kupata hawa marefa wetu, tuache mazoea. Tujenge misingi mizuri kuanzia chini, urefa usiwe kama sehemu ya kupiga deiwaka.

Chanzo: Mwanaspoti