Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni vita ya wabongo ufungaji bora Saudi Arabia

Wabongo Saudia Ni vita ya wabongo ufungaji bora Saudi Arabia

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Clara Luvanga ameendeleza ubabe wake wa kufunga katika Ligi Kuu ya Saudi Arabia na kumfikia mtanzania mwenzake Enekia Kasonga anayekipiga Eastern Flames ya nchini humo

Clara Jana ametia kambani mabao mawili katika mchezo wa Dabi mchezo uliohusisha timu yake ya Al Nassr dhidi ya Al- Hilal, huku wakiibuka na ushindi wa mabao 4-3.

Clara amemfikisha mabao manne katika mechi nne na kuwa sawa mfungaji anayeongoza ligi hiyo mtanzania Enekia Kasongo mwenye mabao manne

Hii inakuwa ni Vita mpya kwa watanzania hao wanaokipiga Ligi Kuu Saudia baada ya kufungana kwa mabao wote wakiwa na mabao manne na wakiwa wamecheza mechi nne

Chanzo: Mwanaspoti