Wakati Simba wakitamba na uwepo wa Kiungo wao Clatous Chotta Chama aliepata kukipiga RS Berkane kama chachu ya kujua mbinu za wapinzani wao kabla ya mchezo wao siku ya Jumapili.
Sasa kwa taarifa yako ndani ya Kikosi cha Wamorocco pia kuna mtu anaeijua Simba kutokana na kucheza nao mara kadhaa katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yule winga wa zamani wa Yanga kwenye kasi ya kishada, Tuisila Kisinda raia wa Congo ambaye sasa anaitumikia RS Berkane, ameipiga mkwara Simba akidai hasira ya kipigo walichopewa na Asec Mimosas zitaishia kwao wakati timu hizo zitakapokutana katika mechi itakayopigwa Jumapili hii.
Kisinda amesema; “Simba nawajua ni wazuri na matokeo waliyoyapata ugenini yamewapa nguvu, lakini nasi tumejipanga na tunataka tu ushindi dhidi yao bila kuangalia idadi ya mabao, tutawapiga.” alisema Kisinda ambaye kasi yake iliwasumbua sana mabeki wa Simba katika Kariakoo Derby.