Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni vita ya mbinu, City vs Tottenham Etihad leo

Pep X CONTE Ni vita ya mbinu, City vs Tottenham Etihad leo

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

(MANCHESTER CITY)

Manchester City wamepoteza michezo minne kati ya mitano iliyopita dhidi ya Spurs katika premier league, wameshinda mchezo mmoja.

Manchester City wameshindwa kupata ushindi katika michezo miwili iliyopita ya premier league, sare dhidi ya Everton 1-1 na kupoteza dhidi ya Manchester United kwa mabao 2-1.

itakuwa ni mara yao ya pili kucheza michezo mitatu mfululizo ya ligi bila kupata ushindi wakiwa chini ya Pep Guardiola baada ya 2016, kama watoshinda dhidi ya Spurs leo.

Pep Guardiola amepoteza mechi tatu zilizopita dhidi ya Antonio Conte katika mashindano yote, hivyo kumfanya kuwa meneja pekee ambaye amekutana naye mara tano au zaiidi kuwa na record bora ya ushindi wa 50% dhidi yake.

Jack Grealish amehusika katika mabao nne kwenye michezo minne ya ligi iliyopita tangu kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia

michezo 4

bao 1

pasi za mabao 3

(TOTTENHAM HOTSPURS)

Tottenham Hotspurs kama watashinda mchezo wa leo, watakuwa timu ya kwanza kushinda michezo mitatu mfululizo ya ligi dhidi ya Pep Guardiola.

Tottenham Hotspurs wamepoteza mechi zote nne za Premier league msimu huu dhidi ya timu zilizo juu yao kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Tottenham Hotspurs wameruhusu mabao mawili au zaiidi katika michezo 11 ya premier league msimu huu, ni Bournemouth pekee ndio wana record mbaya zaiidi wakiwa wamefanya hivyo katika michezo 13 msimu huu.

Harry Kane kati ya mabao yake manne dhidi ya Manchester City katika Premier league, mabao matatu ameyafunga katika dimba la Etihad.

takwimu zake dhidi yao huko Etihad katika michezo ya Premier league

michezo 6

mabao 3

Chanzo: www.tanzaniaweb.live