Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni vita ya Mudathir, Pacome Yanga

Pacome Yanga Cr Ni vita ya Mudathir, Pacome Yanga

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya mzawa Clement Mzize kuibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari wa Yanga, sasa ni vita ya Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua.

Mzize aliwabwaga Gift Fredy na Willyson ambaye amepandishwa kutoka timu ya vijana na alipata nafasi ya kushindanishwa kutokana na kufanya vizuri kwenye mechi za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Mwezi Februari, Yanga inawapambanisha viungo wawili Pacome, Mudathir na beki mmoja ambaye ni Nickson Kibabage.

Kwa mujibu wa takwimu za wachezaji hao watatu kwenye mechi tano za mwezi huo kila mchezaji amefanya kazi kuhakikisha anaipambania timu kupata matokeo mazuri uwanjani.

Mudathir anaongoza akiwaacha kwa mbali Pacome na Kibabage ambapo kwenye mechi tano amefunga mabao manne dhidi ya KMC akifunga mawili Yanga ikishinda 3-0, dhidi ya Mashujaa kafunga moja ikishinda 2-1 na pia kafunga dhidi ya Dodoma Jiji wakishinda bao 1-0.

Wakati Mudathir akiwa na takwimu hizo kwa upande wa Pacome amefunga mabao mawili dhidi ya KMC na Tanzania Prisons Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwa kila mchezo.

Kibabage amehusika kwenye mabao matatu akitoa pasi za mabao mawili ya Mudathir katika mechi na KMC na alitoa pasi dhidi ya Dodoma Jiji bao likifungwa na Mudathir.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: