Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni vilio tu, Wasaudia watakavyoiliza Ulaya kwenye usajili

KDB 2 Ni vilio tu, Wasaudia watakavyoiliza Ulaya kwenye usajili

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati dirisha la usajili la majira ya baridi likiwa linakaribia kufunguliwa kule nchini Saudi Arabia, viroho vya mabosi na makocha wa timu mbalimbali barani Ulaya vimeanza kudunda kwa kasi kwa hofu ya kuwapoteza mastaa wao tegemeo.

Katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi zaidi ya mastaa 10 maarufu walisajiliwa na timu mbali mbali nchini Saudia na wakati wanaondoka kwenye timu zao bado walikuwa wakihitajika kutokana na umuhimu wao.

Timu nyingi zilishindwa kuzuia mastaa hao wasiondoke kutokana na kiasi kikubwa cha pesa ambacho kiliwekwa mezani na matajiri wa Saudi Arabia kama ada ya uhamisho na pesa za usajili.

Mbali ya mastaa ambao waliondoka, wengine walibakia baada ya mazungumzo kuchukua muda mrefu hadi dirisha la usajili nchini Saudia likafungwa.

Hata hivyo mbali ya kufungwa kwa dirisha vigogo kutoka Saudia waliweka wazi kwamba watarudi tena katika dirisha lijalo la majira ya baridi kumalizana na wale ambao walianza nao na kuchukua pia na wingine.

Kilio kinaweza kutokea pale nchini England kwenye Jiji la Liverpool ambapo Al Ittihad ilikuwa tayari kumchukua Mohamed Salah kumlipa mshahara usiopungua Pauni 200 milioni kwa mwaka, huku Pauni 150 milioni ikiwa kama ada ya uhamisho.

Liverpool ilichelewesha mchakato na haikuonekana kuwa tayari kumuuza hadi dirisha likafungwa lakini kwa ripoti za hivi karibuni ni kwamba watu wa karibu wa fundi huyo wamethibitisha kuwa Salah mwenyewe anatamani kuondoka kwenda kuvuna utajiri huo. Na mabilionea hao nao wakiendelea kusisitiza kwamba Januari mwakani watarudi tena kwenye mazungumzo na wawakilishi wa staa huyo raia wa Misri.

Man United imekuwa ikitegemea sana nguvu ya kapteni wao Bruno Fernandez, habari mbaya kwao ni kwamba naye huenda akaondoka kwani Wasaudia walishindwa kumsajili katika dirisha lililopita na kuelekea dirisha lijalo imewekwa ofa ya zaidi ya Pauni 87 milioni kama mshahara.

Huyu akiondoka inaweza kuwa pigo kubwa kwa Man United.

Ukifuatilia tetesi za usajili, timu nyingi zinatamani kumpata straika wa Napoli, Victor Osimhen katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, lakini Wasaudia ambao walishindwa kufanikisha mchakato wa kumsajili kwenye dirisha lililopita ambapo waliweka ofa ya zaidi ya Pauni 50 milioni kwa mwaka huenda wakarudi Januari kumchukua.

Hili halitokuwa pigo kwa Napoli pekee, bali kwa timu nyingi barani Ulaya kama Chelsea ambayo inatafuta straika sambamba na PSG ambayo haina uhakika wa kuwa na Kylian Mbappe katika dirisha lijalo na ilikuwa inamuangalia staa huyu kama mbadala wake.

Mbali ya kwamba wameanza kutafuta mbadala wake lakini litakuwa pigo kwao ikiwa Kevin De Bruyne ataondoka kwenye kikosi cha Manchester City katika dirisha lijalo.

Man City inadaiwa kuwa tayari kumuachia fundi huyu kutokana na majeraha ambayo amekuwa akiyapata mara kwa mara lakini haijapanga kumuachia.

Chanzo: Mwanaspoti