Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni usiku wa Karim Benzema kubeba Ballon D'or leo?

Benzema Ballon D'or 2022 Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema anapewa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo hiyo

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema anatarajiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora Duniani baada ya kuwa na msimu mzuri uliopita kwa kuchukua makombe mbalimbali ikiwemo kombe La UEFA, Taji la ligi kuu na mengine mengi.

Benzema mwenye umri wa miaka 35 alifanya vizuri sana kunako klabu yake ya Madrid huku akiifungia klabu hiyo mabao ya kutosha akiungana na mchezaji mwenzake hatari Viniciouz raia wa Brazil.

Baada ya kukaa muda mrefu bila kuchukua tuzo hiyo ya Ballon d’OR leo hii inawezekana kuwa ndiyo siku maalumu na muhimu kwake kutwaa tuzo hiyo kutokana na kuwa na kiwango bora huku kukiwa hakuna mchezaji aliyeweza kufanya vizuri katika ligi mbalimbali zaidi yake.

Vilevile Real ambayo jana walishinda ushindi mnono baada ya kuitandika Barcelona mabao 3-1 huku Karim akiingia kambani na kuifanya timu hiyo kukaa kileleni huko kwenye msimamo wa Laliga,

Mshambuliaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia klabuni hapo hadi Juni 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live