Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco amesema wataingia katika mchezo wa leo Jioni Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendarmerie Nationale kwa lengo la kutafuta alama tatu lakini ikishindikana watapambana kupata walau alama moja.
Pablo amesema watacheza kwa jitihada muda wote wa mchezo ili kuhakikisha malengo ya kuchukua pointi zote tatu ugenini yanatimia.
Pablo ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu sababu wenyeji Gendarmerie walipoteza mechi ya kwanza hivyo watajipanga kuhakikisha wanatumia vema uwanja wao wa nyumbani.
"Tutaingia katika mchezo wa kesho kwa lengo la kutafuta pointi tatu muhimu ugenini, tusipofanikiwa tutahakikisha tunatafuta sare lakini si kupoteza" amesisitiza Pablo
Simba ipo nchini Niger kukupiga na US gendarmerie katika mchezo wa hatua ya Mkaundi Kombe la Shirikisho Afrika.