Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni nchi gani zisizoitambua Israel?

Ni Nchi Gani Zisizoitambua Israel Ni nchi gani zisizoitambua Israel?

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Takribani nchi 167 kati ya 193 Wanachama wa Umoja wa Mataifa zinaitambua rasmi Israel - Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan, Morocco na Bhutan ni nchi za karibuni zaidi kulitambua taifa hilo - mwaka 2020.

Nchi 28 haziitambui Israel, nyingi ya nchi hizo ni za Kiarabu au zenye Waislamu wengi. Nchi zenyewe ni: Afghanistan, Iraq, Oman, Algeria, Kuwait, Pakistan, Bangladesh, Lebanon, Qatar, Brunei, Libya, Saudi Arabia, Comoro, Malaysia, Mauritania.

Nyingine ni, Somalia, Maldives, Syria, Djibouti, Mali, Tunisia, Guinea, Niger, Venezuela, Indonesia, Korea Kaskazini, Yemen na Iran.

Mei 14, 1948, siku ambayo Mamlaka ya Uingereza kwa Palestina iliisha, Baraza la Kitaifa la Kiyahudi liliidhinisha rasmi tangazo la kutangaza kuzaliwa kwa taifa huru la Israel.

Marekani ilikuwa nchi ya kwanza kuitambua Israel wakati Rais Harry Truman, aliyetawala kati ya 1945 na 1953, alipotoa tangazo la kuitambua dakika kumi na moja baada ya kutangazwa uhuru huo.

Mwaka mmoja baada ya kuanzishwa kwake, Mei 11, 1949, Israel ilikubaliwa kuwa mwanachama wa 59 wa Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.

Chanzo: Bbc