Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni mtukutu Morrison kwa mara nyingine

Morison Niger Wachezaji wa Simba wakishangilia goli la kusawazisha lililofungwa na Morrison

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC imelazimisha sare ya goli 1-1 na wenyeji, Union Sportive Gendarmerie Nationale, mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika uliopigwa dimba la Jénérali Seyni Kountché Jijini Niamey nchini Niger katika mchezo wa pili kwa Simba Kundi D.

Wenyeji, Gendarmerie walitangulia kwa bao la Wilfried Gbeuli dakika ya 12, kabla ya winga Mghana, Bernard Morrison kuisawazishia Simba dakika ya 84.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi nne na kupanda kileleni wakifuatiwa na RS Berkane ya Morocco yenye pointi tatu sawa na ASEC Mimosa ya Ivory Coast, wakati Gendarmerie Leeds inakamilisha mechi mbili bila pointi za inaendelea kushika mkia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live