Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni mchezo mgumu wa Yanga kimahitaji - mchambuzi

Yanga Medeama Ni mchezo mgumu wa Yanga kimahitaji - mchambuzi

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Ibra Kasuga amesema kuwa mchezo wa Medeama dhidi ya Yanga ni mchezo mgumu kimahitaji kwa Wananchi kwani ndiyo utakaoinua morali yao ya kupambana iwapo watashinda au kufifisha matumaini yao iwapo watafungwa.

Kasuga amesema hayo kufuatia mchezo huo wa hatua ya ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa leo huko Kumasi nchini Ghana.

"Mchezo wa Yanga dhidi ya Medeama ni mchezo ambao unaweza ukawakatisha tamaa au ni mchezo ambao inawezekana ukawainua na kurejesha tena matumaini na hata ile fighting spirit ya timu ikaongezeka na kuanza kuamini tena.

"Kwa hiyo kwa mazingira ambayo wapo Yanga na mahitaji ambayo wanayo huu mchezo kwa upande wao unaweza ukasema ni mgumu kimahitaji," Ibra Kasuga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live