Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni kivumbi na jasho EPL tena

EPL Winner Ni kivumbi na jasho EPL tena

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa yanaelekea ukingoni, hivyo mikikimikiki ya Ligi Kuu England inatarajiwa kurudi upya wikiendi hii, ambapo kutakuwa na kipute cha Merseyside Derby na kile cha Chelsea na Arsenal kati ya mechi kali.

Klabu zote 20 zitashuka kumenyana Jumamosi, Jumapili na Jumatatu ili kuonyeshana ubabe baada ya mapumziko ya wiki mbili, kupisha mechi za kimataifa, ikiwamo za kirafiki, kufuzu Euro 2024 na Kombe la Dunia 2026.

Mchakamchaka wa Ligi Kuu England utarudi kwa kipute matata cha mapema, ambapo Liverpool watakipiga na mahasimu wao Everton huko Anfield, Jumamosi.

Kisha Manchester City itajaribu kuweka mambo safi kwa kurejea kwenye makali yake itakapokipiga na Brighton baada ya kupigwa wenye mechi mbili mfululizo, wakati Newcastle United itaikaribisha Crystal Palace kabla ya Chelsea na Arsenal hawajamalizana, Sheffield United wakiwa na shughuli pevu dhidi ya Manchester United.

Ni kivumbi na jasho. Wakati mashabiki wakisubiri utamu huo, makocha wa timu za Ligi Kuu England wanakuna vichwa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi waliopo kwenye vikosi vyao.

Ripoti zinafichua kwamba Chelsea inaongoza kwa kuwa na majeruhi 14, wakati Man United itakosa wachezaji tisa. Liverpool kijasho kinawatoka juu ya ufiti wa staa wao, Andy Robertson wakati Arsenal inasubiri kufahamu hatima ya mkali wao, Bukayo Saka. Hii hapa orodha ya mastaa ambao wapo kwenye hatari ya kukosa mechi za wikiendi hii kwenye Ligi Kuu England kutokana na matatizo mbalimbali.

-Arsenal (4): Jurrien Timber (goti), Bukayo Saka (misuli), William Saliba (mguu), Leandro Trossard (misuli). -Aston Villa (5): Emiliano Buendia (goti), Tyrone Mings (goti), Jacob Ramsey (enka), Alex Moreno (paja) Timothy Iroegbunam (hayupo fiti).

-Bournemouth (7): Tyler Adams (paja), Alex Scott (goti), Emiliano Marcondes (enka), Ryan Fredericks (kigimbi), Lloyd Kelly (kigimbi), Chris Mepham (haijaelezwa), Philip Billing (maumivu) -Brentford (9): Rico Henry (goti), Ivan Toney (adhabu) Kevin Schade (nyonga), Josh Dasilva (paja), Shandon Baptiste (bega), Mikkel Damsgaard (goti), Ben Mee (kigimbi), Lewis Keane-Potter (kigimbi), Mark Flekken (mgonjwa).

-Brighton (6): Julio Enciso (goti), Pervis Estupinan (paja), Jakub Moder (goti), James Milner (haijaelezwa), Tariq Lamptey (haijaelezwa), Kaoru Mitoma (mgonjwa).

-Burnley (6): Michael Obafemi (misuli), Johann Berg Gudmundsson (kigimbi), Manuel Benson (enka), Nathan Redmond (ufiti), Jordan Beyer (maumivu), Hjalmar Ekdal (goti).

-Chelsea (14): Wesley Fofana (goti), Christopher Nkunku (goti), Ben Chilwell (paja), Romeo Lavia (enka), Marcus Bettinelli (goti), Trevoh Chalobah (paja), Reece James (misuli), Cole Palmer (paja), Axel Disasi (paja), Nicolas Jackson (kifundo cha mkono), Armando Broja (haijaelezwa), Benoit Badiashile (paja), Mykhaylo Mudruk (maumivu), Carney Chukwuemeka (haijaelezwa).

-Crystal Palace (11): Eberechi Eze (paja), Nathan Ferguson (paja), Dean Henderson (paja), Jeffrey Schlupp (haijaelezwa), Michael Olise (paja), Jefferson Lerma (paja), Naouirou Ahamada (enka), Matheus Franca (mgongo), Joel Ward (korodani), Cheick Doucoure (paja), Jairo Riedewald (korodani).

-Everton (4): Dele Alli (korodani), Idrissa Gueye (kigimbi), Andre Gomes (kigimbi), Seamus Coleman (goti).

-Fulham (4): Tosin Adarabioyo (korodani), Adama Traore (misuli), Kenny Tete (maumivu), Issa Diop (maumivu).

-Liverpool (6): Curtis Jones (adhabu), Caoimhin Kelleher (goti), Thiago Alcantara (korodani), Stefan Bajcetic (kigimbi), Cody Gakpo (goti), Andy Robertson (bega).

-Luton (6): Albert Sambi Lokonga (paja), Amari’i Bell (paja), Gabriel Osho (goti), Dan Potts (enka), Jordan Clark (enka), Mads Andersen (misuli). -Man City (1): Kevin De Bruyne (paja).

-Man United (9): Lisandro Martinez (mguu), Aaron Wan-Bissaka (misuli), Kobbie Mainoo (enka), Jadon Sancho (adhabu), Amad Diallo (goti), Luke Shaw (misuli), Tyrell Malacia (goti), Sergio Reguilon (misuli), Raphael Varane (haijaelezwa).

-Newcastle (6): Harvey Barnes (mguu), Joe Willock (mshipa wa mguu), Sven Botman (goti), Joelinton (paja), Alexander Isak (korodani), Sandro Tonali (mambo binafsi).

-Nottingham Forest (7): Danilo (paja), Taiwo Awoniyi (korodani), Nuno Tavares (korodani), Felipe (goti), Ola Aina (haijaelezwa), Wayne Hennessey (goti), Serge Aurier (korodani).

-Sheffield United (9): George Baldock (kigimbi), Max Lowe (enka), Ben Osborn (korodani), John Egan (mguu), Chris Basham (mguu), William Osula (haijaelezwa), Rhys Norrington-Davies (paja), Tom Davies (haijaelezwa), Daniel Jebbison (mgonjwa).

-Tottenham (7): Ivan Perisic (goti), Manor Solomon (goti), Ryan Sessegnon (paja), Rodrigo Bentancur (goti), Alfie Whiteman (enka), Yves Bissouma (adhabu), Brennan Johnson (paja).

-West Ham (3): Aaron Cresswell (misuli), Ben Johnson (korodani), Lukasz Fabianski (maumivu).

-Wolves (2): Mario Lemina (adhabu), Hugo Bueno (misuli).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live