Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni hakuna kulala Simba SC

ISRAEL PATRICK MWENDAAAAAA Beki mpya wa Simba, Israel Mwenda akiwa mazoezini na kikosi hicho nchini Morocco

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba, Israel Mwenda ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini wakijifua sambamba na nyota wengine wa kikosi hicho nchini Morocco.

Agosti 16, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ilimtambulisha nyota huyo kwa ajili ya kuwatumikia kwa msimu ujao wa 2021/22 na amesema kuwa yupo tayari kupambana kwa ajili ya timu hiyo.

Picha zilizopo kwenye Mitandao ya kijamii ya Klabu ya Simba, zinamuonesha nyota huyo akishiriki mazoezi, Jambo linalotafsriwa kuwa Simba ni kazi kwa kwenda mbele katika maandalizi yao Msimu Ujao.

Simba SC ndio Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021, na ni Miongoni mwa Timu nne zitakazoiwakilisha nchi Kimataifa katika michuano ya Vilabu Barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live