Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni aibu nzito Simba kuishia Makundi-Ahmed Ally

AHMED ALLY MSEMAJI SIMBA Ni aibu nzito Simba kuishia Makundi-Ahmed Ally

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kwa jinsi Simba SC ilivyo, ni aibu nzito kuishia hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika hivyo, watapambana kuhakikisha wanavuka hatua hiyo.

Ahmed ametoa kauli hiyo leo Marchi 3, 2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya hamasa kuelekea mchezo wao dhidi ya Vipers SC ya nchini Uganda, mchezo utakaopigwa Marchi 7 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Nilishasema na ninasema tena, ni aibu nzito kwa Simba kuishia hatua ya makundi, sisi Simba hatujazoea kuishia hatua hii. Kama utaangalia miaka yote minne tuliyokuwa tunashiriki, mwaka huu tumepata ushindi ugenini hivyo utaona ni jinsi gani bado tunatamani kuvuka.

"Tutafanya kila linalowezekana kuweza kuwafunga Vipers ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini sisi Simba tunafahamu kucheza michezo hii migumu," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live