Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni JKT Queens na wenyeji Abidjan

JKT Queens Vs Abdijan Kikosi cha JKT Queens

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

JKT Queens leo wanashuka tena uwanjani kuikabili Atletico Abidjan ya Ivory Coast kwenye mchezo wa pili wa Klabu Bingwa Afrika huku wachezaji wa timu hiyo wakisema wana matumaini ya kufika mbali na kuchukua ubingwa.

Mechi ya kwanza kwa JKT ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns Ladies, huku Atletico ikitoka sare ya bao 1-1 na SC Casablanca ya Morocco.

Mpaka sasa kwenye kundi A, Mamelodi ndio kinara wa kundi hilo ikiwa na point tatu, Casablanca na Atletico ikiwa na pointi moja huku JKT ikishika mkia bila pointi.

Hii ni mara ya kwanza kati ya timu hizo mbili kukutana kila mmoja ikiambulia sare na kichapo ambapo Mamelodi itakutana na Casablanca.

Kiungo wa JKT, Joyce Lema alisema mechi ya leo watahakikisha hawarudii makosa waliofanya kwenye mchezo uliopita ili kufanikisha malengo yao ya kuchukua ubingwa.

“Sisi hatutakata tamaa, tunaamini Mungu atatusaidia kushinda mechi ya leo na kutimiza malengo yetu ya kuchukua kombe,” alisema Joyce.

Beki wa timu hiyo, Diana Mnally alisema mechi iliyopita walizidiwa ndogo na wababe, Mamelodi Sundowns, hivyo matumaini yataendelea mahali walipoishia katika mchezo huo.

“Kocha amefanyia kazi makosa yaliyopita. Naamini tutafanya vizuri mechi ya leo, hatutakaa kinyonge kwani tuna malengo makubwa, “ alisema Diana.

Chanzo: Mwanaspoti