Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni Express FC Fainali Kagame Cup

SEMI FINAL WINNER Mchezaji wa KMKM FC, akimiliki Mpira mbele ya mchezaji wa Express FC

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama alivyoahidi Kocha wao Wasswa Bossa, Klabu ya Express FC kutoka nchini Uganda imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Michuano ya Vilabu Afrika Mashariki na kati, Cecafa Kagame Cup baada ya kuiadhibu klabu ya KMKM FC kutoka zanzibar.

Express Fc ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 huku gumzo likiwa ni penati ya dakika za lala salama waliyoipata Express FC.

KMKM FC ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 45 lililofungwa na Ibrahim Abdallah,kabla ya Muzamiru kusawazisha dakika ya 56 kwa mpira wa adhabu, kisha kupata penalti dakika za nyongeza iliyowekwa kinywani na kambale ,hivyo kuwapeleka Express hatua ya Fainali wakisubiri mshindi katika mchezo wa Azam dhidi ya Nyasa Big Bullets.

Michuano hiyo itaendelea siku ya Jumatano Agosti 11, kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Pili kati ya Azam FC dhidi ya Nyasa Big Bullets kutoka Malawi katika Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 Usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live