Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ameamua kufunguka ya moyoni kufuatia kiwango kikubwa alichokionyesha mshambuliaji mzawa wa klabu hiyo Chrispin Ngushi ambaye alikuwa anatajwa huenda angepewa mkono wa kwa heri ndani ya klabu.
Ngushi alikuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha kocha aliyepita, Nasreddine Nabi. Kocha Gamondi alimchezesha Ngushi kipindi cha pili kwenye mechi dhidi ya kaizer Chiefs juzi.
"FISTON NGUSHI rudi mbele ya TV yako kisha itazame perfomance yako ya jana (juzi). Hukufunga bao wala hukutoa Assist, Lakini unajua kwanini Mashabiki wanakupongeza?
"Jana ulikuwa wewe. Ngushi yule yule Uongozi wa Yanga uliyemuona kutoka Mbeya Kwanza. Nguvu, kasi, kujiamini na mali mguuni huku ukiwa na maamuzi ya haraka yenye uhakika.
"Na kizuri zaidi umetukumbusha ubora wako kwenye kupiga kwa nguvu kwa miguu yote! Iwe Left au Right, Bakora yako huwa na Power inayofanana. It’s True Yanga Ni Kubwa na Ushindani wa Namba uko kila siku. Lakini hii Haitakiwi kuishi kwenye kichwa chako.
"Hii ni Cancer ambayo Local Players wengi inawamaliza wanapofika kwenye Klabu kubwa. Huja wakiamini wanakuja kuwa PLAN B ya wachezaji wa Nje. Kataa huu ugonjwa Ngushi kutokea jana, rudi kwenye uwanja wa mazoezi na weka jasho lote ardhini.
"Mwalimu ataona, hakuna mfumo wa mpira duniani ukamuacha mchezaji bora mwenye juhudi akiwa Benchi, inawezekana. Nafasi yako inatapatikana. Utacheza zaidi, utazidi kujiamini na Magoli Yatakuja. Huu Ukawe msimu Bora zaidi kwako Straika Chrispin Ngushi," amesema Kamwe.