Prince William amekumbana na busu la shavuni lisilotarajiwa baada ya nyota wa zamani wa Newcastle, Tottenham na Rangers, Paul Gascoigne almaarufu ‘Gazza’ kumbusu shavuni wakati wa ziara yake ya kifalme kwenye duka la Pret A Manger Pret katika mjini Bournemouth leo Septemba 7, 2023.
Gazza (56) ambaye anaishi katika mji wa karibu wa Dorset wa Poole, alikuwa miongoni mwa umati wa watu waliohudhuria ziara hiyo na alilakiwa na Prince William
Gascoigne alikuwa nyota wa timu ya taifa ya England katika miaka ya 1990 ambaye maisha yake ya kibinafsi na mapambano dhidi ya ulevi pia yamekuwa maarufu sana kwenye magazeti Uingereza.
Prince William mwenyewe ni shabiki mkubwa wa soka ambaye pia ni rais wa Chama cha soka la England Chama cha Soka (FA).
Hii sio mara ya kwanza kwa Gazza kufanya tukio hilo bila kutarajia baada ya kumbusu mamake Prince William, Princess Diana mkononi kabla ya Fainali ya Kombe la FA mnamo 1991.
Ziara ya William katika eneo la Pret ilikuwa sehemu ya mradi wake wa Homewards, unaolenga kumaliza ukosefu wa makazi na kuwarudisha watu wasio na makazi kufanya kazi kote nchini Uingereza.